Mke wa mwanamuziki nyota kutoka nchini Marekani Ne-yo, mrembo Crystal Smith mapema July 31, 2022 alitangaza rasmi kuachana na mumewe, ambaye wamedumu naye kwenye ndoa kwa kipindi cha miaka nane na kubarikiwa kupata watoto watatu.

Crystal Smith, ameweka wazi suala hilo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, huku akibainisha dhahiri sababu za kuvunjika kwa ndoa yao kuwa ni kukithiri kwa vitendo vya usaliti bila ya kujilinda kwa kutumia kinga.

Neyo na Mkewe Crystal siku ya harusi yao Resorts World, Las Vegas in 2022 (picha na ET)

Amesema, “Miaka 8 ya uwongo na udanganyifu. Miaka 8 bila kujua kugawana maisha yangu na mume wangu, na wanawake wengi wanaouza miili yao kwake bila ulinzi. Nimeumia moyoni na kuchukizwa ni jambo lisiloeleweka.”

“Kuniuliza nibaki na kukubali ni wendawazimu kabisa, sitadanganya tena umma au kujifanya kuwa hii sio kitu. Ninachagua mimi, ninachagua furaha yangu, afya na heshima yangu. Nilipata watoto 3 wazuri kutokana na hili lakini hakuna kingine bali maumivu ya moyo,” ameandika Crystal.

Ne-yo, ambaye jina lake kamili ni Shaffer Chimere Smith na mkewe Crystal Smith, walifunga ndoa yao mnamo mwaka 2016, ambapo baadaye walitalikiana na mapema mwaka 2020 na baadaye kuweka wazi kurudiana Aprili 2022.

Haji Manara amuangukia Waziri Mchengerwa
Try Again amshukuru Tarimba, SportPesa