Mke wa rais Mstaafu wa Marekani, Barrack Obama, Michelle Obama ametoboa siri jinsi alivyowapata watoto wake wawili na matatizo aliyopitia katika ndoa yake.

Katika kitabu cha Becoming, Bi Obama amefichua kwamba alitokwa na ujauzito na akalazimika kutumia mbinu ya IVF ambapo mayai ya wapendanao huchanganywa nje na baadaye kuwekwa katika kizazi cha mwanamke kupitia sindano.

Michelle Obama ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na kituo cha ABC Good morning America kwamba alihisi amepotea na ni mpweke baada ya kupoteza uja uzito miaka 20 iliyopita.

Aidha, Michelle Obama amesema kuwa walilazimika kufanya vikao vya ushauri na mumewe aliyekuwa rais wa Marekani Barrack Obama.

”Ni muhimu kuongea na akina mama ambao bado ni wachanga kwenye ndoa zao, huu ndio ukweli ulionitokea, nilihisi sina umuhimu wowote tena, mpweke nisiyekuwa na thamani katika dunia hii baada ya kutoka ujauzito,” amesema Michelle Obama

Hata hivyo, Michelle Obama ameongeza kuwa ndoa yao ilikumbwa na misukosuko mara kwa mara hasa baada ya  mumewe kujiunga na bunge, na hivyo basi kumwacha nyumbani ambapo alilazimika kutumia sindano za IVF mwenyewe.

Nikisema Sukuma ndani sitanii, sasa naanza nawewe- RC Tabora
NEC yatoboa siri ya wabunge waliohama Chadema kupita bila kupingwa

Comments

comments