Mke wa waziri mkuu wa Israel, Sara Netanyahu ametozwa faini ya Dola za Marekani 15,000 kwa matumizi mabaya ya fedha za serikali.

Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini Jerusalem imekubali ombi la makubaliano alilosaini Sara Netanyahu na waendesha mashtaka kufikia makubaliano juu ya madai ya kuwa alifuja fedha za serikali kiasi cha dola za Marekani 100,000 kwa kuzitumia kununua vyakula vya kifahari.

Aidha, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka imesema kuwa mke wa Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu atalipa faini ya ziada ili kuhitimisha kesi hiyo, ambayo ili mtuhumu kwa kulipa bili za gharama ya juu za vyakula katika migahawa wakati makazi yake rasmi yalikuwa na mpishi aliyeajiriwa na serikali kutoa huduma kila siku.

Sara Netanyahu alikutwa na kesi ya kujibu ya udanganyifu na kuvunja uaminifu mwaka 2018, huku makubaliano hayo ya kumaliza kesi yalipelekea yeye kukiri tuhuma za makosa mengine madogo madogo na kupunguza kiwango cha matumizi yaliyovuka kiwango kufikia dola 50,000.

Kwa upande wake waziri mkuu wa nchi hiyo, Benjamin Netanyahu anakabiliwa na kesi ya kujibu katika mashtaka tofauti ya ufisadi.

LIVE: Yanayojiri Bungeni jijini Dodoma
Video: Ni lazima kuwe na nidhamu kwenye matumizi ya bajeti- Prof. Lipumba