Mkemia Mkuu ametoa onyo kali kwa mawakala wa forodha wanaogushi nyaraka kwa ajili ya kuingiza kemikali kwani ni kinyume cha Sheria.

Hayo yamesemwa mapema hii leo Jijini Dar es Salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Prof. Samwel Manyele alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uingizaji wa kemikali nchini kutoka nje ya nchi.

Amesema kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Kemikali nchini kila anayeingiza kemikali anatakiwa awe amesajiliwa na kupewa hati ya usajili huo vile vile anatakiwa kupata idhini ya wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali.

“Natoa onyo kwa mawakala wote wa forodha wasiofuata taratibu zilizowekwa na Serikali hasa wanaogushi nyaraka zenye lengo la kukwepesha Sheria na kukwepa kulipa kodi na tozo mbalimbali za Serikali hivyo watakaokaidi hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao,” amesema Prof. Manyele.

Aidha, ameongeza kuwa kuanzia leo Agosti 17, 2017 hakuna mtu atakayeruhusiwa kujishughulisha na shughuli za kemikali bila kuwa na hati ya usajili wa shughuli anayoifanya pia hakuna atakayeruhusiwa kuagiza mizigo ya kemikali bila kuwa na kibali.

Hata hivyo, Prof. Manyele alifafanua lugha elekezi zinazotakiwa kutumika katika kuweka lebo za kemikali husika kuwa ni Kiswahili na Kingereza tu hivyo hakuna kemikali itakayoruhusiwa kuingia nchini ikiwa imendikwa kwa lugha tofauti na hizo.

 

Prof. Mkumbo ampa tano Odinga, asema ni baba wa Demokrasia Afrika
Video: Halmashauri zote zimenyang'anywa mamlaka za kutengeneza barabara-Mdee