Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameupa hadhi ya jiji mkoa wa Dodoma mara baada ya serikali kuhamia mkoani humo.

Ameyasema hayo mapema hii leo wakati wa sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika mkoani humo.

Amesema kuwa mkoa huo kwasasa unastahili kuitwa jiji kwasababu serikali imehamia mkoani humo kwani mkoa huo ni mji mkuu wa Tanzania na uko katikati ya nchi.

“Nimeangalia kuna majiji mangapi Tanzania, Dar es salaam ni jiji, Tanga jiji, Mbeya jiji, Arusha ni jiji, Mwanza ni jiji, kwa hiyo kwa Mamlaka niliyo nayo kuanzia leo Dodoma naipa hadhi ya jiji, hata Meya aliyepo kwa sasa hivi anakuwa ni Meya wa jiji la Dodoma,”amesema Rais Dkt. Magufuli

 

 

Kamati ya saa 72 yaangusha rungu la adhabu
JPM- Tutawashughulikia wote watakao uchezea Muungano awe Nje ya Nchi au Ndani ya Nchi

Comments

comments