Kiungo Gareth Barry anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kukamilisha mpango wa kujiunga na klabu ya West Brom, akitokea Everton kwa ada ya Pauni milioni moja.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 36, anatarajiwa kusaini mkataba wa miezi 12 huko The Hawthorns, na kama ataonyesha kiwango kitakachoridhisha, huenda akasaini mkataba mpya mwishoni mwa msimu huu.

Mwishoni mwa juma lililopita alishindwa kucheza mchezo wa kwanza wa ligi ya England msimu huu akiwa na Everton, kufuatia maumivu wa kifundo cha mguu aliyoyapata akiwa katika mazoezi ya mwisho kabla ya mpambano dhidi ya Stoke City.

Hata hivyo anatarajiwa kucheza mwishoni mwa juma hili akiwa na klabu yake mpya ambayo itapambana na Burnley kwenye uwanja wake wa nyumbani Turf Moor.

Meneja wa klabu ya West Brom Tony Pulis amedhamiria kukamilisha usajili wa Barry kwa ajili ya kuziba nafasi Darren Fletcher aliyetimkia Stoke City katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Endapo mambo yatakua mazuri kama yaanavyotarajiwa, Barry atakua mchezaji wanne kusajiliwa na West Brom katika kipindi hiki, akitanguliwa na Jay Rodriguez, Zhang Yuning na Ahmed Hegazi.

Barry anaendelea kukumbukwa kwa soka safi alilowahi kucheza akiwa na klabu za Aston Villa na  Manchester City, na mpaka sasa ameshacheza michezo 628 ya ligi ya nchini England huku akihitaji kucheza michezo mingine mitano ili kuvunja rekodi iliyowekwa na aliyekua mshambuliaji wa pembeni wa Man Utd Ryan Giggs.

Picha: Umri sio hoja, MC Lyte afunga ndoa
Miikka Mwamba aeleza maajabu ya ‘Balozi DolaSoul’ akiwa studio