Mbunge wa Msalala, Iddi Kassim amechangia hotuba ya bajeti ya Wizara ya Nishati, ambayo iliwasilishwa na Waziri Wizara hiyo, Januari Makamba na kusema mipango iandaliwe kwa kuwapa semina kuwaeleza vijana ni namna gani wanaweza kupata taarifa za kupata mikopo.

Amesema, “kwenye bajeti hii umezungumza, EWURA wametenga fedha kwa ajili ya kuwezesha vijana wetu kuanzisha vituo vya mafuta kwenye maeneo ambayo yana umbali mrefu kwenye vituo hivi vikubwa vya mafuta. Niombe, kwenye maeneo hayo muanze kuandaa semina kuwaeleza vijana ni namna gani wanaweza kupata taarifa za kupata mikopo hii.”

Aidha, katika hatua nyingine Mbunge huyo pia amesema, “kama Wizara hamtaweka jicho katika kuhakikisha kwamba mnadhibiti uingizwaji wa vilainishi feki kwenye nchi hii, tutaendelea kutia hasara kubwa sana wananchi katika maeneo haya” Iddi Kassim, Mbunge wa Msalala.

Dkt. Mpango awakaribisha wawekezaji, asema Tanzania ni salama
Polisi Tanzania: Hatuiogopi Simba SC, tunaiheshimu