Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa atawachukulia hatua watumishi wa serikali ambao wanazuia barua za watumishi wengine hasa walimu wanaotaka uhamisho zisimfikie yeye au Katibu au Waziri Mkuu.

Ameyasema hayo bungeni na mjini Dodoma ambapo amedai kuwa yapo malalamiko ya baadhi ya walimu kushindwa kuhama kutokana na viongozi wao kuzuia barua zao zisifike kwake au viongozi wengine ambao wana mamlaka.

“Mimi ndiyo Waziri wa Utumishi wa Umma nikimbaini kuna kiongozi wa utumishi anakataa kupitisha barua isinifikie mimi, isimfikie Katibu Mkuu Kilimo, isimfikie Waziri Mkuu nitamshughulikia mwa mujibu wa sheria na taratibu,”amesema Mkuchika

Aidha, amesema kuwa zoezi la kuajiri sasa linatarajiwa kuendelea baada ya zoezi la uhakiki wa vyeti feki kukaribia kukamilika na kusema serikali itaendelea na kutoa ajira mpya.

Hata hivyo, ameongeza mwaka jana serikali ilitoa ajira 50,200 na imejipanga kutoa ajira 49,000 kwa ujao.

Video: Diamond Platnumz, Nandy watiwa mbaroni kwa kusambaza video chafu
Diamond ajitoa mkavu, ‘kama sio mimi wa jana vile..’

Comments

comments