Mkurugenzi wa GSM, Hersi Said, amesema kuwa mpango mkubwa wa kuwa wadhamini ndani ya Klabu ya Young Africans ni kuona kwamba siku watakayoondoka wanaacha alama ndani ya klabu hiyo kongwe Afrika Mashariki.

Hayo ameyazungumza jana kwenye ukumbi wa Serena kwenye hafla ya utiliaji saini kati ya Young Africans, La Liga na GSM kuelekea safari ya mabadiliko ambapo mgeni rasmi ni Rais mstaafu wa awamu ya nne.

“Tuna historia ya wadhamini wengi wa Yanga ambao waliwekeza kwa muda siku walipoondoka Yanga iliyumba, sisi hatuna mpango huo tunataka siku tutakayoondoka tuache alama ndani ya Yanga, tuache thamani ili Yanga isimame kwa miguu yake miwili.” Alisema Hersi.  

“Pia La Liga, kupitia Klabu ya Sevilla ya Hispania ni sehemu ya kuitangaza Tanzania kupitia utalii, mafanikio makubwa klabu yetu itapata iwapo tutaweza kushirikiana nao vizuri tutapata nafasi kubwa sana ya kuitangaza nchi yetu,” amesema.

Tayari mkataba wa kuanza safari ya kuelekea kwenye safari ya mabadiliko umeshasainiwa ambapo Mshindo Msolla ambaye ni Mwenyekiti kwa niaba ya Young Africans na Injinia Hersi Said kwa niaba ya GSM.

Tanzania yabaki na wagonjwa wa Corona wanne Pekee
Ligi Kuu: Viporo kuanza Juni 13