Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo John L. Kayombo amefanya ziara ya kushtukiza kwenye kampuni ya New Habari Corparation iliyopo jijini Dar es salaam ambapo miongoni mwa mambo aliyoyakuta ni pamoja na kelele zinazosababishwa na mtambo wa kutengeneza magazeti katika kampuni hiyo ambazo ni hatari kwa wafanyakazi na wananchi wanaoishi eneo hilo .
Kayombo amefanya ziara ya kutembelea katika kampuni hiyo mara baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi na wafanyabiashara wanaoishi jirani na kampuni hiyo.
” Hili jambo sio zuri haiwezekani mashine ipige kelele kiasi hiki huku wafanyakazi wakiendelea kuzalisha magazeti, ni kinyume na haki za binadamu naagiza mashine hii irekebishwe mara moja ili kuondoa hii kero kwa wananchi na wafanyakazi kwa ujumla”Alisema Kayombo
Kwa upande wa wananchi wanaofanya biashara jirani na eneo hilo wamemshukuru mkurugenzi huyo na kusema kuwa kero hiyo imekuwepo kwa muda mrefu na wametoa malalamiko yao lakini hayakufanyiwa kazi.