Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Marekani (CBS) Les Moonves anachunguzwa na shirika hilo mara baada ya kukumbwa na kashfa ya kuwanyanyasa kingono watumishi 6 wanawake wa shirika hilo.

Wajumbe huru kutoka kwenye Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo wanaendela na kazi hiyo tangu Ijumaa ya wiki iliyopita.

Aidha, hisa za Shirika hilo zimeshuka kwa asilimia 6 tangu taarifa zinazomhusu Mtendaji huyo kuanza kusambaa kwenye vyombo vya habari.

Wawekezaji ndani ya Shirika hilo wamepaza sauti wakitaka bwana Les Moonves ajiuzulu nafasi hiyo ili kuokoa hadhi ya CBS

Hata hivyo, taarifa za awali zimebainisha kuwa Wanawake hao walifanyiwa unyanyasaji huo kati ya miaka ya 1980 hadi miaka ya 2000

 

Mke amhubiria mumewe kwenye baa kuacha pombe
Video: Walimu 48 'out' Jangwani, Aliyeachiwa mauaji ya Bilionea Msuya aeleza mazito