Mahakama ya Rwanda imemuhukumu kifungo cha miaka mitano jela aliyekuwa mkurugenzi wa gereza kuu la Kigali kwa kosa la kuiba pesa za mfungwa wa Uingereza.

Innocent Kayumba, ambaye alihukumiwa pamoja na makamu wake wa zamani Eric Ntakirutimana, amekata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, hati ya mahakama inaonyesha.

Mahakama ilimwachilia mfungwa mtaalamu wa IT ambaye alitumia ujuzi wake kudukua kadi ya Visa ya mwathiriwa baada ya kuiambia mahakama kwamba alilazimishwa na mkurugenzi wa gereza kufanya hivyo.

Alisema alitakiwa “kuichambua” kadi iliyohifadhiwa na uongozi wa magereza baada ya kubaini kuwa akaunti ya benki iliyounganishwa nayo ilikuwa na kiasi kikubwa cha fedha.

Mfungwa huyo mwenye uraia wa Uingereza na Misri aliiambia mahakama kwamba zaidi ya £7,000 ($9,300) zilichukuliwa kutoka kwa akaunti yake kwa kutumia kadi yake mwaka jana bila yeye kujua.

Mahakama ilisema Kayumba na naibu wake walipanga njama ya wizi huku mtaalamu wa IT akilazimishwa kuwafanyia kazi, hivyo hakupatikana na hatia.

Kayumba, afisa mkuu wa kijeshi, alihamishwa hadi katika huduma za magereza mwaka wa 2014, akiongoza gereza moja magharibi mwa Rwanda kabla ya kuhamia gereza kuu la mji mkuu.

Kampuni ya mdundo yazindua shindano la Ma DJ 2021
Ukiwa kiongozi una maswali ya kujibu kwa Mungu- Rais Samia