Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli amejitokeza na kuzimaliza tofauti ambazo zilikuwa zimejitokeza katika jimbo hilo huku akiwalaumu viongozi wa vyama kushindwa kutekeleza wajibu wao.

Kagurumjuli ambaye ndiye Msimamizi wa Uchaguzi Kinondoni amesema kuwa baadhi ya vyama wameshindwa kuwapa barua za utambulisho mawakala wao na kutaka kutumia barua za kiapo kama utambulisho.

Amesema kuwa wao kama wasimamizi jukumu lao lilikuwa kutoa barua hizo na pia ni jukumu la viongozi wa vyama kuhakikisha kuwa wanatekeleza wajibu wao kwani huwa ni rahisi kwa wao kukutana na mawakala wao kwani mpaka mawasiliano yao wanakuwa wanayo

Aidha Mkurugenzi huyo ameweka wazi sababu za wao kutoa barua za utambulisho saa tano usiku ni kuhofia barua hizo kugushiwa.

Hata hivyo amethibitisha kuwa dosari hizo zimeshamalizika na hali ya vituo ni shwari hivyo wananchi wasisite kwenda kupiga kura.

Kamanda Mambosasa akiri mtu mmoja kupigwa risasi
Habari Picha: Wananchi wakiendelea kupiga kura Jimbo la Kinondoni