Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, Dkt. Semistatus H Mashimba amekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amepigana na mtumishi wake ambaye ni Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala.

Taarifa zinazosambaa kwenye mitandao zinadai kuwa chanzo cha ugomvi huo ni kumfukuza kwenye nyumba ya Halmashauri mtumishi wake ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi, ambapo amesema jambo hilo halina ukweli wowote.

Mkurugenzi huyo ameitaka jamii kuzipuuza taarifa hizo kwani ni za uongo na hazina ukweli wowote, hivyo amesema taarifa hizo zimetolewa na mtu mwenye nia ovu ya kutaka kufarakanisha viongozi ndani ya Halmashauri na kusababisha taharuki inayochafua utendaji kazi na taswira ya Halmashauri ya wilaya ya Chemba.

Amesema kuwa wilaya hiyo inaendeshwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu pamoja na miongozo inayotolewa na serikali.

Aidha, amesema kuwa uchunguzi unaendelea kufanyika kwa kutumia mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) ili kumbaini mtu aliyeanza kusambaza taarifa hizo ambazo hazina ukweli wowote ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

”Chemba ni Halmashauri ya kazi, Menejimenti na Watumishi wanamahusiano mazuri, wanaendelea na majukumu yao ya kazi katika kuleta maendeleo ya wananchi wa Chemba na Taifa kwa ujumla,”imeeleza taarifa hiyo

Wafugaji waangua kilio mbele ya waziri, asitisha operesheni ya kuwaondoa
Video: Makada sita CCM watajwa kupambana na JPM 2020, Kizungumkuti uchaguzi Serikali za Mitaa