Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu, Volker Turk amesema anatarajia matokeo ya mkutano wa 27 wa nchi wanachama, wa Mkataba wa Kimataifa wa Tabianchi, COP27, utazingatia haki ya kila mtu ya kuishi, ambayo kwa sasa ipo hatarini kutokana na hatua zisizotosheleza za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Geneva, Uswisi na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu kwa vyombo vya habari, imeelezea hatua ya Turk ya kuonya kuwa haki za binadamu ni lazima ziwepo kwenye mazungumzo, ili kupata hatua stahiki za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Baadhi ya Watoto waliokimbia machafufuko huko Kivu Kaskazini, katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Picha: Olivia Acland/ Unicef

Amesema, “Matokeo ya mkutano huo ni muhimu kwa watu wanapaswa kufurahia haki za binadamu kote ulimwenguni, sio tu katika miaka ijayo lakini hata sasa. Watu wanapoteza makazi yao, riziki zao na maisha yao. Kwa kuzingatia mwelekeo wa sasa wa ongezeko la joto, sehemu nyingi ulimwenguni hazitakuwa zinafaa watu kuishi katika kipindi hiki hiki cha Maisha ya watoto wetu, na matokeo yasiyoweza kufikiria.”

Kamishna huyo wa haki za binadamu, pia amesema ukosefu wa haki unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi ni janga na kwamba itachukua miaka mingi kujenga upya na kuanza kuelewa matokeo ya kutokukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, kupunguza athari zake, na kushughulikia matekeo hasi yaliyoathiri Binadamu.

Rais samia azungumza na Waziri Mkuu wa China
Simba SC yazitaka 18 za Novemba