Aliyekua Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga, ameteuliwa kuwa Rais wa heshima wa shirikisho hilo na wajumbe wa mkutano mkuu waliokutana jana jijini hapa.

Jamal Malinzi, Rais wa TFF, aliwasilisha jina la Tenga katika mkutano huo ili wajumbe kulipigia kura na kutokana na mchango wa kiongozi huyo alipitishwa bila kupingwa. Malinzi alisema kwamba kamati ya utendaji ilifikia uamuzi wa kuliwasilisha jina la Tenga kutokana na kuheshimu na kuthamini mchango wake katika soka tangu alipokuwa mchezaji na kiongozi kwenye ngazi mbalimbali ndani na nje ya Tanzania.

Mwenyekiti wa Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), Almasi Kasongo, alitoa sifa za Tenga na kueleza kwamba ameiwakilisha vyema bendera ya Tanzania ndani na nje ya nchi kwa kiwango cha kimataifa.

Kasongo alisema mbali na kuiongoza Taifa Stars katika fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 1980 huko Lagos, Nigeria, Tenga akiwa Rais wa TFF aliweka misingi mizuri ya utawala bora. Rais huyo wa heshima aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania, BMT, Rais wa Baraza la Vyama vya Soka Tanzania (CECAFA) na sasa ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Tenga pia aliwahi kuzichezea Yanga na Pan African zote za Dar es Salaam.

Video Mpya: Dogo Janja - My Life
Antonio Conte Ajiweka Njia Panda