Mkutano Mkuu wa dharura wa ZFA TAIFA umehitimishwa jioni ya leo hii ambapo wajumbe wameazimia mambo mazito.

Ajenda tatu zilijadiliwa katika mkutano huo ambao umefanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo  Kikwajuni Mjini Unguja ambapo miongoni mwa mada tatu zilizojadiliwa, moja  ni kujadili mwenendo wa kamati tendaji ambapo muwasilishaji wa mada hiyo alikuwa Makamu wa Urais ZFA Unguja Haji Ameir (Mpakia), ambaye hata hivyo hakuonekana katika mkutano huo, hivyo, mada yake hiyo ikawasilishwa na Makamu wa Urais ZFA Pemba Ali Mohammed.

Baada ya kusikiliza mada hiyo wajumbe 50 waliokuwepo kwenye ukumbi huo baada ya kuisikiliza mada iliyowasilishwa ambapo walikubaliana kupiga kura, ambayo ilikuwa inamuhusu Makamu wa Rais Unguja, Haji Ameir aliepeleka kesi ya soka Mahakamani mwishoni mwa mwaka 2014. Wajumbe walitaka afukuzwe kwenye chama hicho na asijihusishe na mambo ya michezo kwa muda wa miaka 4.

Wajumbe 50 wakapiga kura ambapo wajumbe 43 walisema afukuzwe na wajumbe 4 walisema asifukuzwe ambapo wajumbe 3 hawakupiga kura.

Hivyo, Alhaj Haji Ameir ambaye ni Makamu wa Urais ZFA Unguja amefutwa rasmi nafasi hiyo na kutojishughulisha na mambo ya michezo kwa muda wa miaka 4.

Aidha mkutano huo umeiondoa kamati ya muda iliokuwa ikiongoza soka la Zanzibar ambapo wajumbe 42 walisema kuwa kamati hiyo iondoke na wajumbe 6 walisema wasiondoke wakati wajumbe 2 kati ya hao 50 hawajapiga kura.

Ajenda ya pili iliyowasilishwa katika mkutano huo kuhusu kuteuliwa Mkaguzi wa Mahesabu yaani ‘Auditors’ kwa ajili ya kuvipitia vitabu vya mahesabu vya Chama hicho ambapo mkutano huo umekubaliana kuchaguwa Kampuni yenye sifa kufanya ukaguzi wa Mahesabu kwa ZFA Taifa ambapo utafanyiwa tangu uongozi wa ZFA wa mwaka 2012 hadi 2016, yani kipindi cha Rais Amani Makungu na Ravia Idarous Faina wa sasa.

Na ajenda ya tatu mkutano mkuu ulikuwa unatakiwa kuamua kuteuwa wajumbe 5 watakaoandika upya Katiba ya ZFA ambapo wajumbe 5 walioteuliwa kati ya 12 waliopendekezwa Awali ni Eliud Peter Mvella kura 46 (Msaidizi mkurugenzi TFF na Mwanasheria), Saleh A. Said kura 43 (Wakili upande wa ZFA),  Affan Othman Juma kura 42 (Kiongozi wa mpira na taaluma ya sheria) Ame Abdalla Dunia kura 40 (Mwalimu/Taaluma ya Sheria), na Othman Ali Hamad kura 36 (Mwanasheria, Kiongozi na mchezaji wa mpira).

Aidha mkutano huo umehalalisha wajumbe waliokuwepo kwenye ZFA Wilaya ya Magharibi “B”  kuwa ni halali na wanatambuliwa na mkutano mkuu na hautofanyika tena uchaguzi kwenye  Wilaya hiyo.

Kuhusu uchaguzi wa ZFA Taifa mkutano huo umetowa tarehe ya kufanyika Uchaguzi huo ambao unatarajiwa kufanyika April 9, 2016 huko Kisiwani Pemba ambapo nafasi ya Urais, Makamu Urais Pemba na Makamu Urais Unguja ndizo nafasi tatu zitagombaniwa katika uchaguzi huo ambapo pia katiba itakayotumika ni ya mwaka 2010.

Jambo jengine katika mkutano huo ni Ligi kuu soka Zanzibar kanda ya Unguja ambayo imeendeshwa na Kamati ya Mpito iliofutwa leo hii, kwa makubaliano ya mkutano huo ligi hiyo wamesema ni halali na wanaikubali, na ligi kanda ya Pemba karibuni itaanza kuchezwa baada ya kukaa kamati tendaji.

Katika mkutano huo Makamu wa Urais Unguja Haji Ameir hakuonekanwa ambapo Kijana Ramadhan Muhsin amekamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kwenda kwenye mkutano huo akiwa si mjumbe wala si mualikwa huku akivaa kitambulisho cha Makamu wa Urais Unguja yani Haji Ameir.

Wanajeshi wa Umoja wa Afrika waingia Burundi
Haya ni Mambo ambayo hupaswi ‘kuya-google’