Mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unatarajiwa kwanza kesho tarehe 27 Novemba 2019  jijini Arusha.

Kuanza kwa mkutano huo kunafuatia kukamilika kwa Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ulioanza Novemba 25 na kumalizika Novemba 26, 2019.

Mkutano wa Makatibu Wakuu pamoja na mambo mengine, umejadili masuala mbalimbali ya utekelezaji ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa mapendekezo kwa mkutano wa ngazi ya Mawaziri wa Wizara za Kisekta zinazohusiana na Jumuiya hiyo utakaoanza  tarehe 27 Novemba 2019.

Washiriki wa Mkutano wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano katika ngazi ya Makatibu Wakuu uliomalizika leo Jijini Arusha

Mkutano huu wa 39 wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umeandaliwa kwa lengo la kujadili na kukubabaliana na agenda zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa 21 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo utakaofanyika Februari, 2020.

Shomari Kapombe atakiwa kurudi Taifa Stars
Dante azua mapya Yanga