Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa SADC, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa wamekubaliana mambo kadhaa katika kikao cha wakuu wa nchi 16 kilichofanyika jana jioni Ikulu jijini Dar es salaam.

Akizungumza hii leo kabla ya kuhitimishwa kwa kilele cha mkutano wa wakuu wa nchi za kusini mwa Afrika SADC, amesema kuwa wameaiagiza Sekretarieti kuanzisha chombo maalum cha kukabiliana na  Majanga ili kusaidia nchi wanachama, zitakapokumbana na majanga kama njaa, mafuriko na magonjwa ya mlipuko.

Aidha, mkutano wa wakuu wa nchi za kusini mwa Afrika ulifanyika jana na leo na ulitanguliwa na maonyesho ya bidhaa katika wiki ya viwanda yaliyoanza Agosti 5 hadi 8 2019 na baadaye ikafuata mikutano ya wataalam pamoja na baraza la mawaziri wa SADC.

”Kwanza wakuu wa nchi wamewapongeza viongozi waliomaliza muda wao kutumikia SADC walipitia hali ya uchumi na kuangalia hali ya majanga,”amesema Rais Magufuli

Hata hivyo, amesema kuwa jambo jingine wameiagiza Burundi iliyoomba kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo, kukamilisha hatua kadhaa kwakuwa kuna baadhi ya vitu havijakamilika.

 

 

NGO's 158 zaondolewa kwenye rejista ya Msajili
Viongozi tisa wa Chadema Mahakamani