Mkuu wa Jeshi la Burundi, Jenerali Prime Niyongabo jana alinusurika kuuawa na watu waliokuwa na silahaa nzito, jijini Bujumbura.

Ripoti zinaeleza kuwa msafara wa Jenerali Nyongabo ulivamiwa na watu wasiojulikana waliofyatua gruneti na makombora na kuwaua watu saba waliokuwa na Jenerali huyo ambaye alishiriki vizuri kuzima jaribio la mapinduzi nchini humo.

Kufuatia tukio hilo, polisi nchini humo limeeleza kuwa watu wawili miongoni mwa washambuliaji hao waliuawa na wengine walikamatwa na maafisa wa polisi.

Hali ya usalama nchini Burundi imeendelea kuwa tete baada ya rais Pierre Nkurunzinza kuwania urais wa awamu ya tatu na kuingia tena madarakani kinyume cha matakwa ya katiba ya nchi hiyo.

Tukio hilo la mauaji ni muendelezo wa matukio ya kushambuliwa kwa majenerali wa jeshi la nchi hiyo kufuatia jaribio la mapinduzi lilifanywa na kundi linalopinga utawala wa rais Nkurunzinza.

 

‘Tanzania Imekosa Viongozi Bora Wa Kuivusha, Nichagueni Mimi’
Siri 5 kubwa Za Mafanikio Bila Utegemezi