Mkuu wa Jeshi la Korea Kaskazini, Jenerali Kim Yong-cholwa ambaye pia ni mtata amewasili Korea Kusini kwa sherehe za kufungwa kwa mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi yanayofanyia huko Pyeongchang.

Jenerali, Kim Yong-chol analaumiwa kwa kuzamisha meli ya vita ya Korea Kusini mwaka 2010 ambapo wanajeshi 46 waliuawa, huku Korea Kaskazini ikikana kuhusika na tukio hilo.

Aidha, familia za waathiriwa na wabunge kadhaa wa Korea Kusini walifanya maandamano wakijaribu kuzuia ziara ya Jenerali huyo.

Wakati wa mashindano ya Olimpiki Korea Kaskazini na Kusini walitembea kwa pamoja chini ya bendera moja wakati wa sherehe za ufunguzi na baadaye wakawa na kikosi cha pamoja na wanawake wa timu ya magongo.

Hata hivyo wachambuzi wa mambo wameonya kuwa kile kinachofanyika kwasasa hakiwezi kumaliza tofauti zilizopo eneo hilo kama Korea Kaskazini haitaacha mpango wake wa majaribio ya silaha za nyuklia.

 

Wakimbizi waandamana na wengine kuuawa nchini Rwanda
Hatma ya Sugu... kuwa huru au kuadhibiwa kesho