Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uganda, Okoth Ochola amewaamuru wananchi kuwakamata au kuwapiga mawe maafisa wa polisi wasiojitambulisha wanapokwenda kuwakamata watuhumiwa hata kama wamebeba bunduki.

Amefikia uamuzi huo mara baada ya vitendo vya utekaji kushamiri nchini humo hivyo jeshi la polisi kuhusishwa moja kwa moja na masuala ya utekaji.

“Afisa wa Polisi anapewa mafunzo jinsi ya kumkamata mtuhumiwa, anastahili kujitambulisha na kumweleza mtuhumiwa sababu za kumkamta kabla ya kumkata. Kama hafanyi hivyo, raia wawakamate au wawapige mawe hao polisi,” amesema Kamanda Okoth Ochola

Aidha, raia nchini Uganda wamesema kuwa wanashindwa kuwatambua wanaowateka nyara jamaa zao, kwani wana tabia sawa na za maafisa wa polisi, wanao wakamata raia bila ya kujitambulisha, wala kuvalia sare za kikazi.

Karibu kila siku, matukio ya mtu kutekwa nyara, hasa wasichana na akina mama yamekuwa yakiripotiwa nchini Uganda.

Hata hivyo, Polisi nchini humo limewakamata wapiganaji wa Mai mai 26 kutoka Jamhuri ya Kidemokraksia ya Congo (DRC), baada kikundi cha wapiganaji hao kuwateka nyara wavuvi 6 raia wa Uganda katika ziwa Edward, magharibi mwa nchi hiyo.

 

Video: Sugu afichua mwanaCCM aliyemtembelea gerezani, Nyumba ya waziri yauzwa kwa mnada
Magazeti ya Tanzania leo Mei 24, 2018