Lesotho, Luteni Jenerali Khoantle Mots’omots’o ameuawawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wenzake waliovamia ofisi yake na kumfyatulia risasi.

Ambapo Waziri mkuu wa Lesotho, Thomas Thabane amesema kuwa mauaji ya mkuu wa kikosi cha jeshi Khoantle Mots’omots’o yaliyofanywa na maafisa wa jeshi ni kitendo ambacho kinarudisha nyuma juhudi za kutafuta amani nchini humo.

Thomas Thabane amesema upelelezi unaendelea juu ya tukio hilo lililotokea katika mji mkuu Maseru siku ya Jumanne.

Mashuhuda wanasema, watu wawili waliovalia sare za jeshi waliingia katika ofisi ya Mots’omots’o na kisha kumfyatulia risasi kabla ya wao kuuawa na walinzi wa kiongozi huyo.

Lesotho ipo katika hali ya taharuki, ikiwa na hostoria ya mapinduzi ya kijeshi ya mara kwa mara.

LIVE BREAKING: Kamati ikitoa taarifa ya uchunguzi wa madini ya Tanzanite, Almasi
Diego Simeone kubaki Atletico Madrid mpaka 2020