Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amemfuta kazi Mkuu wa Magereza nchini humo Wycliffe Ogalo siku chache baada ya wafungwa watatu wanaotumikia kifungo kwa makosa yanayohusiana na ugaidi kutoroka katika gereza lenye ulinzi mkali.

Rais Kenyata amemteuawa brigidia mstaafu John Kibao Warioba kuchukua nafasi ya Wycliffe Ogalo.

Kwa Mujibu wa Msemaji wa Ikulu ya Rais Kanze Dena , Rais Kenyatta amesema nafasi ya Wycliffe Ogalo itachukuliwa mara moja “kuimarisha uwajibikaji katika safu ya uongozi wa vyombo vyote vya usalama”.

Hata hivyo Kenyatta ameagiza mashirika ya usalama kutumia “rasilimali zote zilizopo” kuwasaka waliotoroka.

Waliotoroka ni pamoja na Mohamed Ali Abikar, ambaye alihukumiwa kwa jukumu lake katika shambulio la Chuo Kikuu cha Garissa 2015 ambapo watu 148 waliuawa.

Mtuhumiwa wa pili alikamatwa mwaka wa 2012 kutokana na shambulio lililozuiwa dhidi ya bunge la Kenya na wa tatu kwa kujaribu kujiunga na kundi la wanamgambo wa al-Shabab nchini Somalia.

Mamlaka pia imetoa wito kwa umma, kutoa taarifa kuhusu waliotoroka watatu na kutangaza zawadi ya shilingi milioni 20 za Kenya sawa na ($178,000; £132,000).

Profesa Jay: Wasanii wa sasa hawataki kuhangaika
Pingamizi la Sabaya lakataliwa