Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amesema kuwa amepimwa na kukutwa na virusi vipya vya corona (covid-19), siku tatu zilizopita.

Mkuu huyo wa Mkoa amekaririwa leo, Aprili 29,2020 akisema kuwa hakuwa na dalili zozote za virusi hivyo bali alipima tu kwa lengo la kujua afya yake.

Aidha, amesema kuwa hafahamu ni wapi alipopata virusi hivyo.

Leo, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa idadi ya visa vya corona nchini imefikia 480 na kuwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zaidi.

Corona: Hospitali ya Nairobi kupima sampuli 900 kwa siku, kupima ni Sh 200,000

Mahakama yaamuru Zitto akamatwe

Majizzo afunguka alivyomtoa Jonijoo Wasafi FM, video ya kumtoa jela
Corona: Hospitali ya Nairobi kupima sampuli 900 kwa siku, kupima ni Sh 200,000