Mkuu wa Shirika la Habari nchini Marekani la CBS, Les Moonves amejiuzulu kutokana na kukumbwa na kashfa ya ukatili wa kingono.

Kwa muda mrefu CBS wamekuwa wakimchunguza Moonves tangu zitokee kashfa hizo jijini New York mwezi July mwaka huu na madai mapya dhidi yake yaliyotokea siku ya jumapili dhidi ya wanawake wengine sita.

Moonves mwenye umri wa miaka 68 amekanusha tuhuma hizo na kudai kuwa ni mambo ya kushangaza kuhusiana na tuhuma hizo.

Aidha, kauli iliyotolewa na shirika hilo imesema kuwa Moonves anatakiwa kuachia madaraka kama mwenyekiti, rais na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo haraka iwezekanavyo, ambapo kutokana na kujiuzulu huko Joseph Ianniello kwa sasa atahudumia kama kaimu mkurugenzi mkuu.

Hata hivyo, kwa upande wa Gazeti la Financial Times limeandika kuwa Moonves amejiuzulu kwa kuwa alijua kwamba atatakiwa kulipa fidia nzito ya hadi kiasi cha dola millioni 100 kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani.

Ajali mbaya yaua wanne Kilimanjaro, Rombo
Video: Tazama mwili wa Kofi Annan ulivyopokelewa kwa heshima