Mkuu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini Gambia, Alieu Momar Njai amekimbilia mafichoni mara baada ya rais aliyeshindwa katika uchaguzi uliopita Yahya Jameeh kugoma kuachia madaraka.

Alieu Momar Njai, ndiye aliyetangaza matokeo ya urais kwamba Rais Yahya Jammeh, ameshindwa uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita.

Rais Jammeh, ambaye ameongoza Gambia kwa miaka 22, alishindwa na Adama Barrow katika uchaguzi uliofanyika  Desemba kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.

Aidha, Serikali ya Gambia imevifungia Vituo vitatu vya redio vya binafsi kwa tuhuma za kumkosoa rais huyo kwa kukataa kuachia madaraka.

Juhudi za wanadiplomasia kumshawishi Jammeh, kukubali kung’atuka madarakani lakini mpaka sasa bado hajakubaliana nao.

 

Sheria kuhusu wanawake wawapo kwenye hedhi yazua gumzo Zambia
Nigeria yaanza kugawa fedha kwa raia maskini