Hatimaye Mahakama ya Rufaa ambayo ndiyo ya juu zaidi nchini leo imemhukumu aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kinondoni, Christopher Bageni kunyongwa hadi kufa baada ya kumkuta na hatia katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini.

Bageni amekumbwa na hukumu hiyo kali huku Mahakama hiyo ikiwaachia huru aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO), Abdallah Zombe na wengine wawili waliokuwa washtakiwa katika kesi hiyo iliyodumu kwa muda mrefu.

Uamuzi huo wa Mahakama ya rufaa umekuja kutokana na rufani iliyokatwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kupinga uamuzi wa awali uliofanywa na Mahakama Kuu Agosti 9, mwaka 2009 kuwaachia huru watuhumiwa wote wanne wa kesi hiyo.

Mbali na Zombe na Bageni, watuhumiwa wengine katika kesi hiyo walikuwa ni Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mratibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na Rajabu Bakari.

Katika kesi ya msingi, watuhumiwa walidaiwa kutekeleza mauaji kwa makusudi dhidi ya wafanyabishara wawili wa madini walioingia jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuuza madini hayo. Walidaiwa kutekeleza mauaji hayo Januari 14, mwaka 2006 katika msitu wa Pande jijini humo.

Ahadi za manji kwa timu ya yanga.
Radio 5 yafungiwa miezi 3, yapigwa faini ya sh. mil.5