Mkuu wa wilaya ya Pangani Bi. Zainab Abdallah, ameshangaza ulimwengu  baada ya kumshauri mume wake kuongeza mke wa pili kwa madai kuwa majukumu yake yamekuwa mengi hali iliyopelekea mume wake kukosa huduma za msingi.

”Namshkuru kwa kunielewa na kulifanyia kazi ombi langu, hatimaye nimempata mwenzangu wa kusaidiana naye majukumu mazito ya ulezi wa mume. Alhamdulillah, M/Mungu ametupa riziki na uwezo, hivyo tunapaswa kutumia neema hizi na wengine. Mavazi ya mume wangu nimeyaandaa mwenyewe, yaa rabb atupe stara inshaaAllah.

Kupitia ukurasa wake wa instagram ametoa shukrani kwa mume wake kwa kitendo cha kukubaliana na yeye na kuongeza mke wa pili kitendo ambacho karne hii ni nadra sana kutokea ilihali kuwa dini ya wawili hao inaruhusu utaratibu huo.

“Assalaam Alaykum, nichukue nafasi hii kumpongeza Mume wangu  kwa kuongeza mke wa pili. Kwa kuwa dini yetu ya Kiislam inaruhusu, wazo la kufanya hivyo lilitoka kwangu, kulingana na uzito wa majukumu yangu nalazimika mda mwingi kuwa mbali na nyumbani na hivyo mume wangu kukosa huduma za msingi”, ameandika Bi. Zainab Abdallah.

 

 

Chadema yataka waliokamatwa siku ya maandamano waachiliwe
Mvutano mkali waibuka kati ya Mahakama na Serikali ya Kenya