Wimbo mpya wa Ali Kiba ‘Seduce Me’ ambao umeendelea kupata mafanikio kadiri muda unavyokwenda, umelikuna sikio la Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi na kuamua kumtuza.

Hapi ametumia mtandao wa Instagram kueleza hisia zake baada ya kuiangalia video ya wimbo huo.

“Nimekuelewa sana wa jina@officialalikiba. Kazi imeenda shule. Nidai zawadi kwa muziki huu wa ukweli. Keep the fire burning,” ameandika Hapi akiambatanisha na kipande cha video ya wimbo huo.

Mapema jana, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda pia alionesha kuikubali ‘Seduce Me’ kupitia instagram akiunganisha video hiyo na ya wimbo wa WCB  ‘Zakale’.

Mwingine aliyeinyooshea mikono ‘Seduce Me’ na kueleza wazi kupitia mitandao ya kijamii ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete. 

‘Seduce Me’ imevunja rekodi kwenye YoTube Afrika Mashariki kwa kuangaliwa zaidi ya mara milioni moja ndani ya saa 38.

Video: CCM imejipanga kupata viongozi waadilifu- Polepole
Video: Lissu awataka wanasheria kugoma