Mkuu wa Wilaya ya Iramba, mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais John Magufuli asimuweka kwenye orodha ya Wakuu wa Wilaya wapya atakaowateua hivi karibuni, ikiwa ni siku chache baada ya Rais Magufuli kutaja vigezo vya wateule wake.

Mayenga ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM), aliweka wazi ombi lake kwa Rais Magufuli hivi karibuni alipokuwa akizungumza katika kikao cha Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), mkoani Shinyanga. Alisema kuwa chanzo cha ombi lake ni majukumu mengi yanayomkabiri na kwamba anataka ajikite zaidi katika kusimamia biashara zake binafsi pamoja na majukumu ya ubunge.

“Ombi hili nililitoa binafsi kwa Waziri Mkuu ambaye alinishauri kusubiri uteuzi; isitafsiriwe kwamba nimeogopa kasi ya utendaji ya Serikali ya Awamu ya Tano.Hapana! Nimeona ni vyema nibaki na ubunge na biashara zangu,” alisema.

Mayenga ni mwandishi wa habari kitaaluma na amekuwa Mkuu wa Wilaya wa Kwanza kuweka hadharani kutokuwa na nia ya kuendelea na wadhifa huo kwenye serikali ya awamu ya Tano.

 

 

Nahodha Wa Stars Aliwasili Kabla D’jamena – Chad
Mwandishi wa ‘DW’ aliyetekwa kabla ya uchaguzi wa Zanzibar asimulia yaliyomsibu