Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amelazimika kuwakwepa na kutowasiliana na wafanyabiashara vigogo wa sukari ili asiingie katika mtego wao.

Akizungumza jana  jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wanaotokana na shirikisho hilo, Hapi alisema kuwa amekuwa akipigiwa simu na wafanyabiashara hao hadi usiku wa manane lakini hapokei.

Alisema kuwa baadhi ya wafanyabiashara hao wakubwa wa sukari wamekuwa wakituma jumbe za maandishi kwenye simu yake ya mkononi wakijitambulisha, lakini ameamua kuwakwepa kwani anahofia anaweza kuzungumza nao kisha wakamrekodi na kumuweka kwenye mitandao kwa nia mbaya.

“Sababu ya kwanza sina sababu ya kuzipokea, lakini pili nahofia nikizipokea nitarekodiwa na wafanyabiashara hao na sauti yangu itasambazwa kwenye mitandao, kuonesha nipo pamoja nao,” alisema Hapi.

Alieleza kuwa wafanyabiashara hao wanaweza kuifanya hali ionekane kama yeye anashirikiana nao katika nia yao mbaya ya kuficha sukari inayoua viwanda vya ndani ya nchi.

Serikali yatangaza msako wa waliokula fedha za watumishi hewa
Video Mpya: Madee - Migulu Pande