Mkuu wa wilaya ya Kaskazini B Mkoa wa Ugunja, Rajab Ali Rajab amewataka vijana kudumisha amanina utulivu katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi oktoba.

Akizungumza katika kongamano la vijana wakati Tanzania ikiungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya vijana amesema ili taifa liweze kufikia malengo katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kudumisha amani ni suala la muhimu katika nyanja zote.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema kila mtu ana haki ya kushabikia chama chochote cha siasa lakini ana jukumu kubwa la kudumisha amani na utulivu nchi huku akiwataka vijana kutumia fursa ya kuanzishwa mabaraza ya vijana ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali ikiwemo elimu ya  ujasiriamali.

Sambamba na hayo mkuu huyo wa wilaya amewapongeza vijana wote waliojitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwani imeonesha wazi kuwa vijana wanavyojishughulisha katika sekta tofauti.

TAMWA: wasisitiza uchaguzi huru na haki
Sababu iliyomfanya kubenea asigombee Ubunge