Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara, Sebastian Waryuba ametolea ufafanuzi suala lililoleta sintofahamu kwa jamii la kuwakamata mabinti wanafunzi waliopata ujauzito na kuwapeleka polisi.

Waryuba amesema kuwa amefikia uamuzi wa kufanya hivyo ili kuweza kuisaidia serikali kubaini watu waliosababisha kukatisha masomo kwa mabinti hao, ambao mara nyingi wamekuwa wakihofia kuwataja.

Hata hivyo, ameongeza kuwa mabinti hao pamoja na wazazi wao wametoa ushirikiano wa kutosha kwa serikali kwa kuwataja, huku wakionyesha kujutia baada ya kufikishwa polisi, lakini wote waliachwa huru baada ya kukamilisha mahojiano.

 

Walimu wakuu 30 watumbuliwa
Korea Kaskazini na Kusini zasaka muafaka