Kocha Msaidizi, Charles Boniface Mkwasa amesema ripoti ya vipimo vilivyofanywa na timu ya madaktari imeonyesha baadhi ya wachezaji walikiuka maagizo waliyopewa hivyo kujikuta wakiongeza uzito.

“Programu maalumu tulizowapa zilikuwa na maelekezo, kuna baadhi hawakuzifuata na kabla ya mambo mengine tumewapa programu nyingine ya kupunguza uzito wakati tukiangali nini cha kufanya,” amesema Mkwasa.

Wachezaji waliozidi uzito ni pamoja na David Molinga aliyezidi kilo 12, Yikpe Gislain kilo 10, Said Juma Makapu kilo 6, na Patrick Sibomana kilo 7.

Mkwasa amesema hali ya timu iko vizuri na wachezaji wote wako salama kwani wale waliokuwa na matatizo madogo madogo yamefanyiwa kazi na madaktari na wanaendelea na mazoezi.

Tottenham wakopa mabilioni kuikabili Covid-19
Kinana ageukia uhadhiri masomo ya siasa vyuoni