Mkwasa amesema uwezo wa Hajibu wa kumiliki mpira, kupiga chenga, kufunga mabao na umri mdogo vimemfanya kuendelea kumpa nafasi kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kupambana na Algeria.

“Hajib ni mchezaji mdogo, ana uwezo wa kutosha wa kumiliki mpira, ana mustakabali mzuri. Nimemchukua kwa nia ya kumkuza, kumpa nafasi ya kumjenga Zaidi”.

Hajib alichomoza vizuri msimu uliopita lakini baada ya raundi nane kuchezwa ameonekana kuwa na msaada mdogo kwenye klabu yake ya Simba.

Mkwasa ameongeza kuwa kila mwalimu ana falsafa yake hivyo ataendelea kumpa Hajibu nafasi ya kujifunza kwa .

 “Chipukizi aina ya Hajib wanahitaji muda lakini katika soka letu hatuwapi nafasi, wanapokosea kidogo tu tunawaacha.  Nimeamua kuendelea na Hajibu kwani anahitaji kukuzwa “

Profesa Lipumba Azungumzia Uamuzi Wa ZEC Kufuta Uchaguzi
Lowassa Apinga Rasmi Matokeo ya Urais