Kocha mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa amesema wachezaji watatu aliowasajili kwa ajili ya kuboresha kikosi chake watamsaidia katika lala salama ya Ligi Kuu.

Ruvu Shooting imelitumia dirisha dogo la usajili lililofungwa rasmi Januari 15, kuwasajili mabeki wawili Haji Mwinyi Mgwali kutoka KMKM, Edward Manyama akitokea Namungo na James Msuva kutoka KMC.

Kocha Mkwasa amesema kila mchezaji aliyemsajili ndani ya kikosi chake ana manufaa makubwa na anajua viwango vyao vitaisaidia timu hiyo.

“Mfano Manyama ni moja ya mabeki wazuri katika ligi, beki mzuri wa kushoto najua atanisaidia kwa kushirikiana na akina Juma Nyoso nitakuwa ba safu imara zaidi ya ulinzi.”

“Hata Mgwai pia ni moja ya mabeki wazuri amecheza Young Africans muda mrefu na hata timu ya taifa hivyo uwezo wake ni mkubwa.” Amesema Kocha Mkwasa.

Ruvu Shooting inashika nafasi ya tano  kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na alama 28, zilizotokana na ushindi katika michezo saba kupoteza michezo mitatu na kuambulia sare saba.

TPLB: Ligi Kuu Kuendelea Februari 13
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 21, 2021