Malimi Busungu, Elias Maguri pamoja na viungo wa Simba na Azam, Jonas Mkude na Salum Abubakar wameongezwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kitakachoivaa Algeria kwenye mechi ya kusaka tiketi ya kufuzu kombe la Dunia.

Kocha wa Taifa Stars, Boniface Mkwasa ameteua kikosi cha wachezaji 28 kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya mtoano wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya timu ya taifa ya Algeria.

Kutokana na udhaifu ulionekana kwenye idara ya kiungo kwenye mechi dhidi ya Malawi, Mkwasa amewaongezea viungo Jonas Mkude wa Simba na Abubakar Salum wa Azam kujaribu kuimarisha safu hio.

Salim Mbonde wa Mtibwa Sugar na Hassan Kessy wa Simba wameongezwa kwenye safu ya ulinzi huku mshambuliaji wa Stand United, Elias Maguli akijumlishwa kusaidia safu ya ushambuliaji.

Malimi Busungu wa Yanga ameongezwa kwenye kikosi hicho kuongeza changamoto kwenye idara ya ushambuliaji huku Rashid Mandawa na Deus Kaseke wakipoteza nafasi zao baada ya kutoitwa.

Tarehe 14 mwezi ujao, Taifa Stars itakuwa mwenyeji wa Algeria  katika pambano la mtoano wa kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi. Mechi ya marudiano itachezwa tarehe 17 nchini Algeria.

Kikosi kamili: Walinda Milango: Ally Mustafa (Yanga), Aishi Manula (Azam), Said Mohamed (Mtibwa Sugar),

walinzi wa pembeni : Kessy Ramadhani, Mohamed Hussein (Simba), Juma Abdul, Haji Mwinyi (Yanga) na Shomari Kapombe (Azam),

Walinzi wa kati: Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub (Yanga).

Viungo: Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar, Himid Mao, Mudathir Yahya, Frank Domayo (Azam), Jonas Mkude na Said Ndemla (Simba)

Washambuliaji wa pembeni: Farid Musa (Azam), Simon Msuva (Yanga) na Mrisho Ngasa (Free State Stars – Afrika Kusini).

Washambuliaji wa kati: John Bocco (Azam), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim Hajibu (Simba), Malimi Busungu (Yanga), Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – Congo DR).

Song Kupanga Mikakati Dhidi Ya Taifa Stars
Matokeo Jimbo la Kawe, Ubungo, Kigamboni na kuhusu Kibamba kwa Mnyika