Kocha mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya Jumatatu katika uwanja wa taifa, jiojini Dar es Salaam kuisapoti timu hiyo itakapomenyana na Chad.

Taifa Stars jana ilishinda 1-0 Uwanja wa Omnisports Idriss Mahamat Ouya mjini D’jamena dhidi ya wenyeji, Chad katika mchezo wa Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika, bao pekee la Mbwana Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji.

Na vikosi vyote, Chad na Tanzania vitasafiri leo kuja nchini (Dar es Salaam) kwa ajili ya muendelezo wa michezo ya kuwani kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kupitia kundi H, ambapo kuna timu nyingine kama Nigeria pamoja na Misri.

Akizungumza baada ya mchezo wa jana, Mkwasa kwanza aliwapongeza vijana wake kwa kazi nzuri hadi kupata ushindi huo, licha ya kucheza kwenye mazingira magumu ya joto kali.

“Tulikuwa na dakika 90 ngumu sana, joto kali na jua pia, lakini tunamshukuru Mungu tumeshinda na sasa tunaelekeza akili zetu kwenye mchezo wa marudiano Jumatatu,”amesema.

Ushindi wa jana unaifanya Tanzania ifikishe pointi nne baada ya mechi tatu, kufuatia kufungwa 3-0 awali na Misri mjini Cairo na kulazimishwa sare ya 0-0 na Nigeria Dar es Salaam mwaka jana.

Chelsea Wambembeleza Baba Yake Mats Hummels
Waziri Maghembe amtumbua Mkurugenzi Wanyamapori kwa kuvusha Tumbili