Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ amewapa nafasi ya kusomba mbele Azam FC, katika Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Azam FC wameshindwa kufurukuta nyumbani na kuambulia matokeo ya sare ya 0-0 dhidi ya Miamba ya Misri Pyramids FC katika mchezo wa Mkondo wa Kwanza, Uwanja wa Azam Compex Chamazi jijini Dar es salaam.

Mkwasa ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter kuwa: ” Inawezekana kabisa Azam FC ikashinda ama kupata sare ya Mabao kule Misri, matokeo ambayo yatawavusha kwenda hatua inayofuata.”

“Hata hivyo namna walivyocheza leo, hawashawishi kama watafanya hilo.”

“Wanahitaji kuwa na kiwango bora na bahati kubwa na mno kule Misri ili waitoe Pyramids FC.”

Mchezo wa Mkondo wa Pili kati ya Pyramids FC dhidi ya Azam FC utachezwa mwishoni mwa juma lijalo mjini Cairo, Misri.

Serikali yatenga Bilioni 45 kutekeleza anwani za makazi nchini
TPLB, ZPLB zakutana Dar