Mlinda mlango Goran Lenac ambaye alikuwa akikipiga katika klabu ya Fc Bolekj inayoshiriki katika ligi kuu nchini Montenegro amepigwa risasi.

Inadawaiwa kwamba Goran Lenac alikuwa katika uwanja wa mazoezi wa klabu yake ya Fc Boelkj ambapo alikuwa akifanya mazoezi na marafiki zake kabla ya tukio hilo la mauaji kujitokeza.

Wakati akiendelea kufanya mazoezi na wachezaji wenzake kulitokea kundi la watu walikuja na kufyatua risasi kadhaa zilizompiga kichwani huku wakifyatua nyingine hewani ili kuwakaimbiza watu waliokuwa wakitazama mazoezi.

 

Baada ya tukio hilo Polisi waliweka vizuizi katika mji wa Kotor ili kuwazuia watu wasitoke na Lenac alikimbizwa hospitali lakini tayari alishapoteza uhai.

Nchi ya Montenegro ni nchi iliyoko Kusini Mashariki mwa Ulaya lakini ni kati ya nchi ambazo ulinzi wake uko chini sana na imetawaliwa sana na matukio.

Gazeti la Mwanahalisi lafungiwa kwa uchochezi
Gigy Money ataja sababu ya 'Papa' kufanya vizuri