Kufuatia matokeo ya Kidato cha nne kutangazwa siku chache zilizopita na kuonesha kuwa shule nyingi za serikali kufanya vibaya Mbunge wa Ulanga (CCM) Goodluck Mlinga ametoa ya moyoni na kumchana Waziri wa Elimu, Profesa. Joyce Ndalichako na kusema kuwa hafai kuendelea kushika nafasi hiyo.

Mlinga amesema shule za Serikali zimezidi kufanya vibaya katika mitihani ya Taifa huku shule za watu binafsi zikionyesha kufanya vyema zaidi na kudai bila shule binafsi Waziri Ndalichako angekuwa Waziri wa Masifuri.

“Suala langu la kwanza ni ushukaji wa elimu kwa shule za Serikali za Tanzania, kwa muda wa miaka miwili sasa Waziri wa Elimu amedumu katika wizara hii lakini tumeshuhudia uangukaji mkubwa wa shule za sekondari za serikali hivyo Mhe. Ndalichako anaweza kujipima mwenyewe kwa kiasi gani ni mzuri na kiasi gani ni mbaya na hii inanipa hofu sijui Maprofesa wa Tanzania wanatatizo gani?.

Hivyo Mlinga amemshauri Rais Magufuli amchague Msukuma au Lusinde ambao wameishia darasa la saba kuwa Mawaziri wa Elimu kwa sababu wanajua matatizo gani mpaka wakashindwa kusoma.

Mliga ameongezea kuwa “Mwaka huu matokeo ya shule za sekondari za serikali katika shule bora 10 hakuna na sisi tulizoeaga kusikia Mzumbe, Kilakara lakini saizi hazipo na katika shule 100 bora za sekondari shule za serikali zipo nne tu jamanii hii si aibu, Waziri wa Elimu una kitu gani cha kutuambia sasa maana umeonyesha kufeli halafu ukija unawapiga vita watu wenye shule binafsi, sasa kwa mfano hizi shule za binafsi tungeziondoa kwenye orodha ya zile shule 100 bora wewe si ungekuwa Waziri wa masifuri? Ehh angekuwa waziri wa masifuri maana shule za sekondari za serikali zote zimefeli”.

Mbali na hilo Mlinga aliweka wazi kuwa shule za sekondari ya serikali zinapata matokeo mabovu kutokana na mazingira mabovu ya shule zenyewe kuanzia kwa walimu kwani walimu hao muda mrefu wanaidai serikali malipo yao na wamekuwa hawalipwi kwa kigezo cha serikali kusema wanahakiki, lakini pia amedai walimu wanapangiwa vijijini sehemu ambazo hazina miundombinu mizuri.

Odinga azungumzia kumtoa Kenyatta Ikulu
Kiongozi wa upinzani Zimbabwe akabidhi mikoba