Afya njema ni kitu cha kwanza katika maisha ya wanadamu wengi na paale unapopata tatizo la kiafya huwa mawazo mengi yakuja kichwani haswa ukifikiria kua malengo ya kimaendeleo uliyojiwekea yatasimama.

Mbunge wa ulanga Godfrey Mlinga amelionaa suala hilo na kuweka kuwa kipaumbele chake ndani ya miezi sita ya mwanzo amekwisha nunua gari la kubebea wagonjwa lakini bado amedhamiria kuhakikisha kuwa kila tarafa y jimbo lake kwenye kituo cha afya kutakuwepo na garihilo (ambulance).

Akifanya mahojiano na Ayo Tv Mbunge  huyo aliyejizolea umarufu kwa kutaka serikali ifikirie kuhusu kuchongwa sanamu ya Diamond na mtindo wake wa uwasilishaji hoja amesema anahitaji kufanya hivo ili kupunguza vifo vya wajawazito kwa kuchelewa kufika katika vituo vya afya.

Hata hivyo Mlinga amesema kwamba anataka kuhakikisha elimu inapatiwa kipaumbele ili kuongeza ufaulu ambao katika jimbo lake ni hafifu huku kukiwa na ukosefu wa mashine za uchapishaji na walimu wakiwa wanaandika mitihani ubaoni.

”jimbo langu ni kubwa sana lakini kuna changamoto kama stationary hakuna hivyo walimu wanaandika mitihani ubaoni, nitaligawanya katika tara kuu nne na kuweka vituo vya kuchapisha mitihani nataka kuwa mbunge wa mfano na wa kukumbukwa, nataka kuboresha elimu ndani ya jimbo langu.

.

Matokeo ya Ualimu (DSEE) na GATCE 2016
Kajala Amkumbusha Binti yake Jukumu Alilopatiwa na Babu Seya katika Siku yake ya Kuzaliwa