Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Job Ndugai amewatahadharisha baadhi ya wabunge waliokuwa wanamtuhumu kuwa mdhaifu katika kufanya maamuzi kwa kusema kuwa kwa sasa wataona dhahiri udhaifu wake uko wapi.

Ameyasema hayo mara baada ya kuanza kwa kikao cha kwanza cha mkutano wa 8, wa Bunge la 11, mjini Dodoma wakati akiwakaribisha wabunge 7 wapya wa Chama cha Wananchi (CUF) waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi kuchukua nafasi ya wabunge nane ambao walivuliwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge.

“Taratibu zote zilifuatwa kwa wabunge hawa kuingia hapa bungeni, wapo baadhi ya lile kundi wiki mbili kabla ya mambo haya kutokea walisema Spika dhaifu, nikasema sasa udhaifu wangu ndiyo utaonekana. Kama una akili yako maneno kama haya hayana umuhimu,”amesema Ndugai

Aidha, Spika Ndugai amewakaribisha wabunge walioapishwa huku akiwafunda wabunge hao, kuwa kiapo walichokula wenzao leo kiwa kumbushe utii na uaminifu kwa tiba ya nchi

Hata hivyo, Wabunge hao walioapishwa leo wanatarajiwa kupangiwa kamati ili waanze kazi mara moja, kama ambavyo Spika amewataka kufanya hivyo.

Mtoto wa Lil Wayne awatoa hofu mashabiki
Marekani yaishangaa Korea Kaskazini kutaka vita