Hatimaye aliyekua beki wa kati wa Simba SC Yusuph Mlipili amepata timu ya Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kuachwa na mabingwa hao wa Tanzania Bara mwanzoni mwa msimu huu 2020/21.

Mlipili ambaye Singida United iliyoshushwa madaraja mawili, amejiunga na Kagera Sugar inayonolewa na kocha mzawa Mecky Mexime, anatumainiwa kuwa msaada mkubwa kwenye kikosi cha klabu hiyo, ambacho kinaendelea kupambana kwenye Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Beki huyo kijana amesaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo ya mkoani Kagera, na rasmi ametambulishwa kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za Kagera Sugar.

Usajili wa Mlipili unakua wa kwanza kwa Kagera Sugar kwenye dirisha dogo ambalo lilifunguliwa rasmi Desemba 16 na kutarajiwa kufungwa Januari 15 mwaka 2021.

Hata hivyo usajili wa Mlipili kwenda Kagera Sugar umewashutua wadau wengi wa soka, kufuatia tetesi kudai alikua na mpango wa kujiunga na Wagosi wa Kaya (Coastal Union), lakini mambo yamekwenda tofauti.

Ikumbukwe kuwa Mlipili aliachwa na Simba SC kutokana na kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha miamba hiyo ya Msimbazi, huku ingizo jipya Kened Juma likitajwa kuwa kikwazo na kupelekea kocha Sven apendekeze aachwe.

Mlipili ni miongoni mwa wachezaji wazawa ambao waliweza kufanya vizuri ndani ya Simba SC zama za kocha Patrick Aussems ambaye alikuwa akipenda kuwaanzisha na pacha wake Erasto Nyoni.

Magufuli awanyooshea kidole TRA
Wabunge wa Republican wafungua kesi dhidi ya Pence