Mlipuko wa lori la mafuta uliotokea katika eneo la magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, umesababisha vifo vya watu 12 na majeruhi ambao idadi yake haikuweza kupatikana mara moja baada ya kuungua na moto walipokuwa wakijaribu kuchota mafuta.

Ajali hiyo, ambayo bado haijaelezewa kwa kina chanzo chake, ilitokea katika barabara ya kitaifa 1, karibu na kijiji cha Mbuba, kilichopo eneo la Madimba kilomita 120 magharibi mwa Kinshasa ambapo gari hilo lilikuwa likielekea likielekea Kinshasa na lililipuka karibu na soko dogo.

Mama akipita jirani na Lori hilo lililopata ajali na kuwaka moto jirani na soko la Madimba, DRC. Picha na Th Guardian.com

Mara baada ya ajali hiyo, Gavana wa Kongo ya Kati, Guy Banduisema alichapisha andiko kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa, “Watu kadhaa wamefariki na kuchomwa moto sana Mbuba jioni ya leo baada ya lori la mafuta kulipuka kwenye eneo la RN-1.”

Chapisho hilo lilisema, “Ni zaidi ya huzuni na wakati wa kuchukua hatua kali na za ujasiri ili kuimarisha udhibiti wa usafiri ni sasa, na hii maalum kwa bidhaa zinazoweza kuwaka moto, ili kukomesha mzunguko huu wa majanga na wala RN1 haipaswi kuwa kaburi.”

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Septemba 17, 2022    
Waliofariki kwa mafuriko, shoti ya umeme wafikia 134