Serikali ya Korea Kusini imetangaza hali ya dharura, kutokana na mlipuko wa moto mkubwa wakwanza kutokea katika historia ya nchi hiyo.

Moto huo umepelekea zaidi ya watu 4,000 kuhamishwa makazi na hadi sasa tayari mtu mmoja ameripotiwa kufariki.

Moto huo umewaka katika milima ya kaskazini mashariki mwa korea kusini karibu na mpaka wa korea kaskazini, ambapao tayari maelfu ya wanajeshi, mainjinia wa moto zidi ya 800 kutoka maeneo yote ya Korea kusini wameungana na vikosi vya zima moto ili kukabiliana nao.

Taarifa za awali kutoka kwa uongozi zinaeleza kuwa japo moto huo mkubwa umesha dhibitiwa kwa kiasi kikubwa, hasa kwenye kiini lakini bado kuna maeneo ambayo hawajayafikia na yanateketea

Wameongeza kuwa wana amini moto ulianza jana usiku katika eneo la Spark lililokuwa na transfoma karibu na mji wa Gangwon kaskazini mwa Seoul.

Kutokana na upepo mkali uliokuwepo katika eneo hilo ulipelekea moto huo kuenea kwa kasi ya haraka kuelekea katika maeneo ya mlimani ambako maonesho ya Olimpiki ya mwakajana yalifanyika hapo

Rias wa nchi hiyo Moon Jae-in, tayari ameitisha kikao cha dharura na viongozi wa srikali yake ili waone ni namna gani wanaweza kukabiliana na janga hilo lililo pelekea mamia ya makazi kuteketea na waziri wa ulinzi ametuma wanajeshi 16,500, ndege za kivita 32 na magari 26 ya zimzmoto kutoka jeshini.

Kwa mara ya mwisho janga la moto kuikumba nchi ya Korea kusini ilikuwa mwaka 2007, baada ya bomba la mafuta machafu kupasuka na kumwaga maelfu ya tani za mafuta Baharini.

Video: Makonda atoa msaada wa milioni kumi kwa Wajane
Jokate afunguka mafanikio kampeni ya tokomeza zero, mamilioni yakusanywa