Jeshi la Marekani limethibitisha kutokea kwa mlipuko nje ya uwanja wa ndege wa Kabul nchini Afghanistan huku Marekani ikiendelea na zoezi la kuhamisha maelfu ya watu kutoka uwanja huo.

Akielezea kuhusu mlipuko huo Msemaji wa Makao Makuu ya jeshi la Marekani Pentagon, John Kirby amesema bado haijafahamika moja kwa moja kama kuna watu waliokufa kwenye mlipuko huo.

Hata hivyo Mataifa ya Magharibi yalikuwa tayari yameonya juu ya uwezekano wa shambulio katika uwanja wa ndege wa Kabul katika harakati za kuhamisha watu, Nchi kadhaa zilitoa wito kwa raia wake kuepuka maeneo ya uwanja wa ndege, ambapo maafisa wamedai kulikuwa na kitisho cha bomu la kujitoa muhanga.

Waziri wa mambo ya nje Antony Blinken alikadiria kwamba karibu Wamarekani 1,500 bado wanasubiri kuhamishwa katikakati mwa ongezeko la tahadhari za kitisho cha ugaidi katika uwanja wa ndege

Aidha Afisa wa kundi la Taliban ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa watu wasiopungua 13 wakiwamo watoto wameuawa na kwamba askari kadhaa wa Taliban pia wamejeruhiwa katika mlipuko huo.

Simba SC kurejea Dar
PICHA: Miquissone atambulishwa rasmi Al Ahly