Takribani watu saba wameripotiwa kufariki dunia huku wengine 13 wakijeruhiwa baada ya mlipuko mlipuko kukumba msikiti wa waumini wa dhehebu la Shia wakati wa ibada ya Ijumaa katika mji wa Kandahar nchini Afghanistan.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba mlipuko huo ulitokea katika msikiti wa Imamu Bargash ambapo idadi kubwa ya watu wameuawa.

Hata hivyo chanzo cha mlipuko huo hakijatajwa licha ya kwamba kuna tuhuma za mlipuaji wa kujitoa mhanga aliyeshiriki katika ibada hiyo.

Kundi la wapihganaji wa Talibani liliteka mji wa Kandahar, mji wa pili kwa ukubwa nchini Afghanistan Agosti 13 baada ya vita vikali

Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC nchini humo Secundar Kermani kupitia ukurasa wake wa Twitter alindika kuwa kundi la IS-K, Tawi la Islamic State nchini humo linatarajiwa kutangaza kwamba ndilo lililohusika na shambulio hilo.

Neema yawashukia wakazi wa Siha
Pyramids FC: Tutacheza kwa tahadhari kubwa