Raia wa Marekani mwenye asili ya Tanzania amekamatwa jijini Dodoma akidaiwa kuingia nchini na kukwepa kukaa karantini, kinyume na maagizo ya Serikali.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amesema kuwa walimkamata mtu huyo juzi akiwa amepanda usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda.

Alisema kuwa baada ya kumhoji alikiri kuingia nchini na kudai kuwa alijiweka karantini ya hiari nyumbani kwao.

“Nyumbani kuna chumba maalum cha mtu kujihifadhi. Kwahiyo nilipofika nilijiweka karantini kwa siku 14 na baadaye ndipo nikatoka,” mtu huyo alijieleza mbele ya Mkuu wa Wilaya.

DC Katambi ameeleza kuwa mtu huyo atafanyiwa uchunguzi chini ya timu ya watalaamu wa afya ili kubaini afya yake pamoja na mambo mengine.

Jana, Serikali ilitangaza kuwa wasafiri wote wanaoingia nchini watakaa katika hostel za Chuo Kikuu Cha Dare es Salaam maarufu kama Hostel za Magufuli. Lengo ni kuhakikisha wanawekewa ulinzi ili kuepuka baadhi ya walioripotiwa kutoroka kabla ya kukamilisha siku 14.

Gonzalez ajinyonga baada ya kukutwa na Corona
R.Kelly amlilia Jaji amtoe jela, ahofia virusi vya Corona

Comments

comments